Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Prof. Mabula Daudi
Mchembe amefaya ziara ya kutembelea Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Geita unaotekelezwa na TBA kama Mkandarasi na Mshauri Elekezi. Akiwa katika
eneo hilo la Mradi amefurahishwa na jinsi TBA inavyoendelea na hatua za
umaliziaji wa ujenzi wa baadhi ya Majengo katika eneo hilo.
Vile
vile Prof. Mchembe aliongeza kusema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Wizara ya
Afya na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ni mzuri hivyo kurahisisha utekelezaji
wa mradi huu.
Aidha,
Meneja wa TBA Mkoa wa Geita Mhandisi Gradys Jefta alieleza kuwa Ujenzi wa
Hospitali hiyo umefikia asilimia 91% ya utekelezaji na kuahidi kuendelea na
kazi za umaliziaji ili mradi huu uweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutowa
huduma kama ilivyopangwa.
Kwa upande wa Msimamizi wa Mradi Mbunifu Majengo Grace Elias alisema Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita unazingatia viwango vya ubora katika kila hatua ya utekelezaji. Aliongeza pia kuwa vifaa vyote vinavyotumika katika ujenzi vikiwemo nondo, zege, maji, mchanga na vingine huwa vinapimwa kabla ya kutumika ili kudhibiti viwango vya ubora wa jengo linalojengwa.