Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Oktoba 18, 2020 amehudhuria hafla ya kumkabidhi Rais wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi nyumba maalum ya kuishi iliyojengwa na Serikali eneo la Masaki jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo Mhe. Rais Magufuli aliwapongeza TBA kwa usimamizi mzuri pamoja na kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo kwa gharama nafuu.
Vile vile Rais Magufuli alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete unaoendelea eneo la Kawe ambao unatekelezwa na TBA kama Mkandarasi na Mshauri Elekezi.
Ujenzi wa nyumba hizo ni kwa mujibu wa sheria namba 3 ya mwaka 1999 inayo ainisha ujenzi wa nyumba maalum kwa ajili ya makazi ya waheshimiwa Marais wastaafu.