Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

DKT. MSONDE APONGEZA TBA, AHIMIZA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIRADI YA PPP

Imewekwa: 05 August, 2026
DKT. MSONDE APONGEZA TBA, AHIMIZA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIRADI YA PPP

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, leo Agosti 5, 2026 ametembelea banda la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, jijini Dodoma, na kupongeza kazi zinazofanywa na wakala katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Serikali.

Akiwa katika banda la TBA, Dkt. Msonde amesema Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TBA imefungua fursa mpya za uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini kupitia utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP), hatua inayolenga kuongeza uwekezaji na kuchochea maendeleo ya sekta ya ujenzi na uchumi wa taifa.

Amesema TBA imeendelea kuwa chombo muhimu katika utekelezaji wa miradi ya Serikali, huku ikitoa nafasi kwa sekta binafsi kushiriki katika maendeleo ya miundombinu ya majengo kupitia mfumo wa ubia.

Hivi karibuni, TBA ilitangaza maeneo 38 yaliyopo katika mikoa 20 nchini ambayo yameiva kwa utekelezaji wa miradi ya ubia (PPP). Maeneo hayo yanafaa kwa uwekezaji katika miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi, hoteli, majengo ya biashara, maduka pamoja na maeneo ya mapumziko.

Dkt. Msonde amewahimiza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia fursa hizo kwa kushirikiana na TBA katika kuendeleza miradi yenye tija kwa uchumi na maendeleo ya wananchi.

Aidha, amepongeza jitihada za TBA katika kusimamia na kutekeleza miradi ya ujenzi wa majengo ya Serikali pamoja na miradi ya ubia, akibainisha kuwa hatua hizo zinaunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi jumuishi, shindani na endelevu.

Amesema ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kupitia miradi ya PPP ni miongoni mwa mikakati muhimu ya kuharakisha maendeleo ya miundombinu, kuongeza ajira na kuvutia uwekezaji nchini.

slot gacor