Lengo
kuu la Wakala ni kutoa huduma ya makazi kwa serikali na watumishi wa
umma pamoja na huduma ya ushauri kwa majengo ya serikali. Majukumu ya
Wakala ni kama ifuatavyo:
Ujenzi
wa nyumba mpya za serikali
Matengenezo
ya majengo ya serikali
Uuzaji
wa nyumba za serikali kwa Watumishi wa Umma
Upangishaji
wa nyumba za serikali kwa Watumishi wa Umma na upangishaji baadhi ya
nyumba za serikali kibiashara.
Kusimamia
miradi ya ujenzi na kutoa huduma ya ushauri kwa majengo ya serikali
Kutoa
ushauri kwa serikali kuhusiana na masuala yote yahusuyo nyumba