
UJUMBE WA MTENDAJI MKUU
Kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), napenda kukukaribisha kwenye tovuti yetu rasmi. Tovuti hii ni jukwaa muhimu la mawasiliano kati ya TBA na Wadau mbalimbali kama wananchi, wadau wa maendeleo, taasisi za Serikali, na taasisi binafsi. Hapa utapata taarifa sahihi na za kina kuhusu huduma zetu, miradi tunayotekeleza, mafanikio yetu, pamoja na mikakati mbalimbali tuliyonayo juu ya uendelezaji wa sekta ya ujenzi hususani majengo.
Kama taasisi ya Serikali iliyopewa dhamana ya kusimamia ujenzi na ukarabati wa majengo ya Serikali nchini, TBA inaendelea kuwa mshirika muhimu katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika nyanja za elimu, afya, kilimo, teknolojia, biashara, makazi, na utawala bora. Tunajivunia kuwa chombo chenye wataalamu waliobobea na wenye uzoefu wa kutosha katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa majengo ya Serikali kwa kuzingatia viwango vya ubora na thamani ya fedha.
Kupitia tovuti hii, tunakukaribisha na kukuhamasisha kufuatilia taarifa zetu, kutoa maoni yako, na kushirikiana nasi kwa njia ya uwazi na uwajibikaji. TBA inaendelea kujidhatiti kuhakikisha kuwa inachangia kikamilifu katika maendeleo ya Taifa letu kupitia ujenzi wa miundombinu bora ya majengo hapa nchini.