Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

MAFUNZO ELEKEZI KUONGEZA TIJA YA UTENDAJI KAZI KWA WAAJIRIWA WAPYA TBA

Imewekwa: 10 October, 2025
MAFUNZO ELEKEZI KUONGEZA TIJA YA UTENDAJI KAZI KWA WAAJIRIWA WAPYA TBA

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kwa kutekeleza Sera ya Mafunzo katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2013 umeandaa mafunzo elekezi kwa Waajiriwa wapya wa TBA ambayo yameendeshwa na Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Meneja wa Fedha na Hesabu TBA CPA (T) Ally Kiko amesema kuwa ni matarajio ya Wakala kwamba elimu waliyoipata waajiriwa wapya itakuwa chachu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi chote watakachokuwa wakihudumu katika Utumishi wa Umma.

Aidha, waajiriwa wapya wameushukuru uongozi wa TBA, Chuo cha Utumishi wa Umma pamoja na wawezeshaji wa mafunzo elekezi kwa kufanikisha mafunzo hayo ambayo yataleta tija na kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni za Utumishi wa Umma.

Aidha, mafunzo Elekezi kwa waajiriwa wapya 24 yamefanyika kwa siku 4 kuanzia Oktoba 07 na kuhitimishwa leo Octoba 10, 2025 jijini Dar es Salaam.