Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN WATEMBELEA MIRADI YA TBA JIJINI DAR ES SALAAM

Imewekwa: 29 July, 2025
WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN WATEMBELEA MIRADI YA TBA JIJINI DAR ES SALAAM

Wawekezaji kutoka Japan wakiambatana na Wataalam kutoka TBA wametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika ziara hiyo Mshauri Mtendaji kutoka Kituo cha Ujenzi cha Japan Dkt. Izumi Hiroto amesema "Jana tulikuwa na Semina yenye mafanikio na leo tumefanya ziara ya kutembelea miradi ya TBA na NHC. Tumetembelea Miradi miwili ya TBA na nimevutiwa kwa jinsi walivyotekeleza miradi hii kwani wametekeleza kwa kushirikiana na sekta binafsi. Ushirikiano wa namna hiyo unaleta faida kwa pande zote mbili hivyo, namna hii ya mashirikiano inaweza hata kuwavutia wawekezaji wageni. Makampuni ya kijapani yamekuja hapa kwa lengo la kutafuta fursa za uwekezaji katika sekta ya majengo hata hivyo, mfumo wa TBA ni mfumo mzuri kwa mgeni anayehitaji kuwekeza nchini Tanzania”

Aidha, wawekezaji hao walitembelea Mradi wa nyumba za Makazi za Magomeni Kota awamu ya I na II; Chimala Pamoja na Mradi wa Canadian Masaki. Ziara hiyo imefanyika leo Julai 29, 2025 Jijini Dar es Salaam.