Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

WANANCHI MBALIMBALI WA SEKTA YA UJENZI WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA TBA SABASABA 2026 JIJINI DAR ES SALAAM

Imewekwa: 08 July, 2026
WANANCHI MBALIMBALI WA SEKTA YA UJENZI WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA TBA SABASABA 2026 JIJINI DAR ES SALAAM

Wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi wameendelea kujitokeza kwa wingi kutembelea banda la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), kufuatia tangazo la fursa za uwekezaji kupitia ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP).

TBA imetangaza fursa za uwekezaji katika maeneo 38 yaliyopo katika mikoa 20 nchini, yatakayowekezwa kwa mfumo wa ubia. Fursa hizo zinahusisha ujenzi wa nyumba za makazi (apartments), majengo ya biashara, maduka, hoteli pamoja na vitega uchumi vingine vinavyolenga kuchochea maendeleo ya sekta ya ujenzi na ukuaji wa uchumi wa Taifa.

slot gacor