• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • English

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaWakala wa Majengo Tanzania

  • kuhusu Sisi
    • Ujumbe kutoka kwa Mtendaji Mkuu
    • Sisi ni Nani
    • Dira na Dhamira
    • Tunafanya Nini
    • Mikakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Bodi ya Ushauri
    • Muundo wa Taasisi
    • Senior Management
    • Kurugenzi wa Uwezeshaji wa Huduma
    • Kurugenzi ya Ushauri
    • Kurugenzi ya Ujenzi
    • Kurugenzi ya Miliki
    • Meneja wa Mikoa
  • Nyumba
    • Nyumba za Kuuza
    • Nyumba za Kupangisha
    • Fomu ya Ununuzi wa Nyumba
    • Fomu ya ununuzi wa Nyumba
  • Miradi
    • Miradi Tunayoishikilia
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyo Katika usanifu
    • Miradi Tunayotegemea kufanya
  • Machapisho
    • Machapisho
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
  • Ununuzi
    • Mpango wa Manunuzi wa Mwaka
    • Mialiko ya zabuni
    • Orodha ya Wazabuni Walioshinda

Habari Mpya

  • SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWENYE UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI

    tokea mwezi 1
  • MENEJIMENTI YA TBA YAHIMIZWA KUKUTANA MARA KWA MARA.

    tokea mwezi 1
  • TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

    tokea mwezi 1
  • TBA NA ZBA KUENDELEZA MASHIRIKIANO

    tokea mwezi 1

Latest Press Release

WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA NYUMBA ZA MAGOMENI KOTA AWAMU YA PILI.

Imewekwa: Wednesday 24, July 2024

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ameitaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha nyumba za makazi zinazosimamia wapangaji wote wanalipa kodi kwa wakati pamoja na kukusanya madeni kwa wadaiwa sugu kwa kufata sheria za mikataba ili fedha hizo zitumike katika ujenzi wa majengo mawili kwa ajili ya watumishi wa Umma (Block C na D,) Magomeni Kota awamu ya pili ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 15.

Akizungumza leo Julai 23, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla ya Ufunguzi wa Nyumba za Makazi zilizojengwa na TBA katika eneo la Magomeni Kota Awamu ya pili ‘B’ lililogharimu shilingi Bilioni 5.6 Mhe. Bashungwa amesema kuwa Serikali imeendelea na jitihada za kujenga makazi bora kwa watumishi ili kupunguza changamoto za makazi.

Amesema kuwa na watumishi waliopata fursa ya kuishi katika nyumba hizo kutimiza wajibu kwa kulipa kodi kwa wakati ili kuiwezesha TBA kujenga nyumba nyingi zaidi katika mikoa mbalimbali nchini kwa kuwa uhitaji wa nyumba bora umefikia zaidi ya nyumba milioni tatu kwa ongezeko la nyumba laki tatu na tisini elfu kila mwaka.

Ameelekeza Wakala hiyo kuendelea kufanya kazi kiwango bora na ubunifu zaidi kwa wakati huu ambao Serikali imerekebisha sheria ya Wakala kwa kutoa fursa kwa TBA kushirikiana na sekta binafsi pamoja na Taasisi za fedha katika uendelezaji milki, kujenga nyumba za makazi kwa watumishi wa Umma pamoja na watanzania kwa ujumla.

Aidha ameipongeza Wakala hiyo kwa kuwa wabunifu katika ardhi na mipango ya majengo ya kisasa katika miradi wanayoisimamia, ambapo katika eneo la Magomeni lenye hekari 32 awali lilikuwa na wakazi 645 na baada ya TBA kusimamia ujenzi na ukadiriaji majengo ekari 9 zimejengwa nyumba za makazi zilizotosheleza wakazi 645.

“TBA inakwenda katika mwelekeo sahihi katika ubora wa majengo pamoja na teknolojia ikiwemo hii ya kitasa janja itakayosaidia kuwadhibiti wanaokwepa kulipa kodi…..TBA chukueni hatua kwa wadaiwa sugu bila kuangalia wadhifa.” Ameongeza Bashungwa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro amesema mradi huo umegharamiwa na Serikali kwa fedha za ruzuku zipatazo shilingi Bilioni 5.687 na utekelezaji wake ulianza Novemba 2022.

Amesema jengo hilo ni la pili kati ya majengo 5 yanayojengwa katika eneo hilo kwa ajili ya makazi ya watumishi wa Umma ambapo jengo moja tayari limekamilika na limepangishwa na hadi kukamilika kwa majengo yote matano jumla ya kaya 80 zitakuwa zikiishi hapo, Na ujenzi wake umezingatia kanuni na misingi ya ujenzi wa majengo ya Serikali.

“Jengo A limekamilika na tayari limepangishwa, jengo B ni hili ulilolizindua leo na majengo mawili C na D ujenzi wake umefikia asilimia 15 na ukamilishaji wa majengo hayo yaliyosalia kadiri ya mpango kabambe uliopo utategemea upatinaji wa fedha.” Amesema.

Kuhusiana na ubunifu unaofanywa na Wakala hiyo Kondoro amesema; ujenzi huo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM,) ya 2020/2025 ibara ya 55 (h) inayoelekeza maeneo yaliyorejeshwa Serikali Kuu chini ya Wakala hiyo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kuendelezwa kwa kujenga nyumba zinazoweza kubeba familia nyingi (apartments.) bora na za kisasa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema, uzinduzi huo ni matokeo mazuri ya utendaji kazi TBA chini ya Wizara ya Ujenzi ambao wamekuwa wakitekeleza miradi kwa teknolojia ya ubora na upangaji wa miji.

“Nyumba hizi msiwape wahuni, wanaofanya kazi ya udalali na baadaye kuleta taharuki za madai ya kodi kubwa na gharama nyingine na kuharibu taswira ya eneo hili, nyumba hizi zinapangishwa kwa gharama ndogo ikilinganishwa na kodi ya soko.” amesema.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge amesema, wameridhika na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na TBA katika Manispaa hiyo kwa kuwa imeboreshwa kwa kuzingatia mipango miji na mradi huo wa nyumba za watumishi wa Umma umezidi kupendezesha Manispaa ya Kinondoni pamoja na kupunguza changamoto ya makazi.

Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

TBA
THE CHIEF EXECUTIVE, TANZANIA BUILDINGS AGENCY (TBA), 13 MOROGORO ROAD, P.O BOX 94, 41102 VIWANDANI, DODOMA TANZANIA, EMAIL: ce@tba.go.tz Website: www.tba.go.tz
Nukushi :
Namba ya Simu : +255 733 483 437, +255 677 108 010
Barua Pepe : barua@tba.go.tz

Linki za Haraka

Linki Linganifu

  • WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Utumishi
  • Tume ya Takwimu ya Taifa
  • Tume ya Ajira

©2025 wakala wa majengo tanzania . Haki zote zimehifadhiwa..

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.Inaendeshwa na Wakala ya Majengo Tanzania