Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

WAZIRI KADOGOSA AITAKA TBA KUTUMIA MALI ZAKE KUONGEZA UWEZO WA UWEKEZAJI NA KUJITEGEMEA KIFEDHA

Imewekwa: 10 November, 2026
WAZIRI KADOGOSA AITAKA TBA KUTUMIA MALI ZAKE KUONGEZA UWEZO WA UWEKEZAJI NA KUJITEGEMEA KIFEDHA

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kungu Kadogosa, leo Novemba 09, 2026, ametembelea Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na kusisitiza umuhimu wa taasisi hiyo kutumia kikamilifu rasilimali na mali ilizonazo, kuimarisha uwekezaji pamoja na kushirikisha sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi yake ili kuongeza uwezo wa kifedha na kufikia azma ya kujitegemea.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya TBA jijini Dar es Salaam, Mhe. Kadogosa ameitaka Bodi na Menejimenti ya TBA kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza thamani ya mali za taasisi, kukamilisha zoezi la uthamini wa mali zote na kutumia rasilimali hizo kuvutia mitaji kupitia taasisi za kifedha na masoko ya mitaji.

Mhe. Kadogosa amesema kuwa zoezi la uthamini wa mali zilizopo katika baadhi ya mikoa limeonesha kuwa TBA ina rasilimali zenye thamani kubwa ya kiuchumi. Amesisitiza kukamilishwa kwa uthamini wa mali zote ili kuwezesha Wakala kutumia rasilimali hizo kama nyenzo ya kuimarisha uwezo wake wa kifedha na kuendeleza miradi ya uwekezaji.

Aidha, ameitaka TBA kushirikisha sekta binafsi kupitia utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ili kuongeza mitaji, ufanisi na kasi ya utekelezaji wa miradi. Pia amesisitiza Bodi na Menejimenti kuwa wabunifu na kushughulikia changamoto za taasisi kwa kushirikiana na Wizara, hususan za kisera na kisheria.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), FRV. Said Mndeme (ndc), amesema kuwa Wakala umepokea maelekezo ya Waziri na umejipanga kufanya mageuzi ya kimkakati yatakayoharakisha kufikia lengo la kujitegemea kifedha.

Amesema TBA inamiliki maeneo ya uwekezaji yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi na yaliyopo katika maeneo ya kimkakati nchini. Ameeleza kuwa Wakala utaimarisha ushirikiano na wawekezaji, wakandarasi na taasisi za kifedha kupitia mifumo ya ubia ili kuyaendeleza maeneo hayo na kuongeza mapato.

Ameongeza kuwa Menejimenti itaendelea kufanya mageuzi yatakayoiwezesha TBA kutumia fursa za uwekezaji zilizopo, kuimarisha uwezo wa kifedha na kufikia azma ya kujitegemea.

 

 

slot gacor