KAMATI YA BAJETI YA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA) YAKAA KIKAO
KAMATI YA BAJETI YA WAKALA WA MAJENGO TANZANIA (TBA) YAKAA KIKAO
Imewekwa: 14 August, 2025

Kamati ya Bajeti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imefanya kikao cha kujadili mwenendo wa mapato ya Wakala kwa kipindi cha mwezi Julai 2024 hadi Juni, 2025.
Aidha, kikao hicho kiliweza kuwasilisha na kujadili mkakati wa ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa mpango kazi wa Wakala kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026 pamoja na kuwasilisha na kujadili mapendekezo ya matumizi kwa mwezi Julai, Agosti na Septemba, 2025.
Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ndogo za TBA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.