Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

TBA NA BENKI YA AZANIA WASHIRIKIANA KUPANUA FURSA ZA UPATIKANAJI WA MIKOPO YA NYUMBA TANZANIA

Imewekwa: 09 July, 2026
TBA NA BENKI YA AZANIA WASHIRIKIANA KUPANUA FURSA ZA UPATIKANAJI WA MIKOPO YA NYUMBA TANZANIA

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Benki ya Azania zimetia saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa mikopo ya nyumba kwa Watanzania, hatua inayotarajiwa kupanua fursa za wananchi kumiliki makazi bora na kuchochea maendeleo ya sekta ya nyumba nchini.

Kupitia ushirikiano huo, Benki ya Azania itatoa huduma za kifedha ikiwemo mikopo ya nyumba kwa wateja wa TBA, ili kuwawezesha Watanzania kumudu gharama za ununuzi wa nyumba zinazojengwa na Wakala.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania, Bw. Yahaya Mbanka, amesema ushirikiano huo unaakisi dhamira ya benki hiyo ya kuwasaidia Watanzania kutimiza ndoto ya kumiliki nyumba kupitia huduma rafiki za kifedha.

“Makubaliano haya ni zaidi ya ushirikiano wa taasisi mbili. Ni hatua muhimu ya kurahisisha upatikanaji wa mikopo ya nyumba na kuwawezesha Watanzania kutimiza ndoto ya kumiliki makazi bora kupitia suluhisho rafiki za kifedha. Tunaamini huduma za kifedha zinapaswa kubadilisha maisha ya watu na kuchangia maendeleo ya Taifa,” amesema Bw. Mbanka.

Ameongeza kuwa Benki ya Azania itaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu na bidhaa zake za mikopo ya nyumba, sambamba na kubuni suluhisho za kifedha zinazokidhi mahitaji ya makundi mbalimbali ya wananchi.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud W. Kondoro, amesema makubaliano hayo yataongeza uwezo wa wananchi kupata mikopo ya nyumba kwa urahisi zaidi, hivyo kuimarisha umiliki wa makazi bora na kuongeza mafanikio ya miradi ya makazi inayotekelezwa na TBA.

Ameeleza kuwa utekelezaji wa ushirikiano huo utaanza katika mradi wa makazi wa TBA unaoendelea eneo la Masaki, jijini Dar es Salaam, ambapo nyumba 370 zinatarajiwa kujengwa.

Arch. Kondoro ameishukuru Benki ya Azania kwa kukubali kuingia katika ushirikiano huo wa kimkakati, akisema TBA itaendelea kushirikiana na taasisi za kifedha na wadau mbalimbali ili kuongeza upatikanaji wa makazi bora, kuimarisha ustawi wa wananchi na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Taifa.

 

 

slot gacor