Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

TBA YAVUTIA WANANCHI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Imewekwa: 18 June, 2026
TBA YAVUTIA WANANCHI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

 Juni 17, 2026, ni siku ya ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, wananchi mbalimbali wanaendelea kutembelea banda la Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili kupata huduma, elimu na taarifa kuhusu majukumu pamoja na miradi inayotekelezwa na wakala huo.

Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete. Mwaka huu, maadhimisho hayo yanaongozwa na kauli mbiu isemayo, “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.”

Mbali na kutoa huduma kwa wananchi, TBA inatumia Maonesho haya kama fursa ya kutangaza na kuhamasisha uwekezaji katika miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi

Wakala huo umeainisha maeneo kadhaa yenye fursa za uwekezaji na unaendelea kuwakaribisha wawekezaji kushirikiana katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa kushirikiana na sekta binafsi pamoja na taasisi za kifedha.

Lengo lingine la maonesho haya pia ni kutatua kero na changamoto za kiutumishi kwa watumishi wanaotembelea Maonesho haya.

slot gacor