Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

MKURUGENZI WA HUDUMA SAIDIZI WA TBA ATEMBELEA BANDA LA TBA KATIKA MAONESHO YA 50 YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABASABA)

Imewekwa: 13 July, 2026
MKURUGENZI WA HUDUMA SAIDIZI WA TBA ATEMBELEA BANDA LA TBA KATIKA MAONESHO YA 50 YA KIMATAIFA YA BIASHARA (SABASABA)

Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Bi. Amina Lumuli, leo Julai 13, 2026, ametembelea banda la TBA katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) na kujionea miradi mbalimbali ambayo Wakala umekuwa ukiitambulisha kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda hili.

Miongoni mwa miradi iliyowasilishwa ni ujenzi wa nyumba za makazi na maduka ya biashara katika maeneo ya Ghana Kota, Mwanza na Canadian, Masaki jijini Dar es Salaam, pamoja na miradi mingine ya ujenzi, ushauri wa kitaalamu na usimamizi wa miradi ambayo TBA imeitekeleza katika maeneo mbalimbali nchini.

slot gacor