Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

WAHANDISI TBA WAPATIWA MAFUNZO YA PROGRAMU YA PROTASTRUCTURE 2026

Imewekwa: 12 August, 2025
WAHANDISI TBA WAPATIWA MAFUNZO YA PROGRAMU YA PROTASTRUCTURE 2026

Wahandisi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wamepatiwa mafunzo ya ngazi ya pili ya programu ya Protastructure 2026 yaliyotolewa na Nziza Global Tanzania  yenye lengo la kuwaongezea ujuzi mkubwa katika usanifu wa majengo marefu kwa kuzingatia hali ya hewa (upepo na matetemeko ya ardhi).

Mafunzo hayo yametoa fursa kwa Wahandisi wa TBA kujifunza kwa vitendo namna ya kufanya usanifu wa mihimili ya majengo (High rise Buildings), kutatua changamoto za uandaaji na usanifu wa miundombinu ya majengo zinazoukabiri ulimwengu kwa kutumia zana za hivi karibuni za Protastructure. Hata hivyo, Mafunzo hayo yaliyofanyika yataongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi kwa wahandisi katika kutekeleza majukumu yao na kuboresha kwa zaidi ya 40% kasi ya utoaji huduma na kwa ufanisi zaidi hasa kwa miradi mikubwa na tata.
Aidha, mpango huu wa mafunzo unaunga mkono lengo linaloendelea la TBA kutumia teknolojia za kisasa ili kuboresha ubunifu, kupunguza muda wa kukamilisha miradi na kukuza mtiririko wa kazi uliojumuisha kada za ujenzi ili kufanikisha uandaaji wa michoro kwa muda uliyokusudiwa.

Mafunzo hayo ya ngazi ya pili ya programu ya Protastructure 2026 yameendeshwa kwa muda wa siku tano na Nzinza Global Tanzania katika ukumbi wa Grand Villa Kijitonyama kuanzia Agosti 04 hadi 08, 2025 Jijini Dar es Salaam.