Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

WATAALAM TBA WASHIRIKI SEMINA YA MAKAZI, UJENZI NA MAENDELEO YA MIJI

Imewekwa: 28 July, 2025
WATAALAM TBA WASHIRIKI SEMINA YA MAKAZI, UJENZI NA MAENDELEO YA MIJI

Wataalam kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wameshiriki semina ya Makazi, Ujenzi na Maendeleo ya Miji kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wawekezaji katika sekta ya Miliki kutoka Japan.

Akizungumza katika semina hiyo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali inaalika wawekezaji katika sekta ya Miliki kutokana na ongezeko la huitaji wa Makazi unaochagizwa na kukua kwa kasi kwa Miji nchini.

“Serikali tumeshachukua hatua kubwa sana ya kuhakikisha kwamba mwekezaji yeyote hata wawekezaji wa ndani wanaotaka kuingia katika sekta ya Miliki wanaingia kiurahisi” aliongeza Mhe. Ndejembi.

Aidha, Afisa Miliki Mwandamizi kutoka TBA Bw. Marco Silabi amesema kuwa mabadiliko ya sheria ya uanzishwaji wa Wakala yaliyofanyika 2023 yameruhusu TBA kujiendesha kibiashara na hivyo semina hiyo imewawezesha kufanya mazungumzo na wawekezaji hao juu ya namna ya kuendeleza Miliki za TBA na kusaidia Taifa kwa ujumla.

Semina ya Makazi, Ujenzi na Maendeleo ya Miji imefanyika leo Julai 28, 2025 katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.