Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

WATAALAM WA TBA WAPATA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA GRMS

Imewekwa: 28 July, 2025
WATAALAM WA TBA WAPATA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA GRMS

Watalaam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wamepata mafunzo ya matumizi sahihi ya mfumo wa Usimamizi wa Miradi na Miliki za Serikali ( GRMS) yaliyotolewa na wawezeshaji kutoka Kitengo cha TEHAMA TBA.

Katika mafunzo hayo wataalam wamefundishwa namna ya kuingiza taarifa za miradi katika mfumo huo pamoja na kuweza kutengeneza namba ya malipo (control number) kwa ajili ya malipo ya miradi mbalimbali.

Aidha, mfumo huu unatarajia kuweka uwazi katika utekelezaji wa miradi, kurahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za miradi kidigitali, kuongeza mapato ya Wakala pamoja na kutunza kumbukumbu sahihi ya miradi ya washitiri mbalimbali.

Mafunzo hayo yametolewa leo katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Ofisi ndogo za TBA Makao Makuu Jijini Dar es Salaam.