Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

TBA YAELEZA JINSI UWEKEZAJI WA MITAMBO UNAVYOPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI

Imewekwa: 05 August, 2026
TBA YAELEZA JINSI UWEKEZAJI WA MITAMBO UNAVYOPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umesema uwekezaji wake katika mitambo na mashine za kisasa umeendelea kuongeza ubora wa miradi ya ujenzi, kupunguza gharama za utekelezaji na kurahisisha shughuli za ujenzi katika maeneo mbalimbali nchini.

Meneja wa Kitengo cha Mitambo na Mashine wa TBA, Mhandisi George Chaula, amesema hayo wakati akielezea mikakati ya wakala katika uwekezaji wa mitambo na mashine kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.

Amesema TBA imewekeza katika mitambo mbalimbali ya kisasa inayotumika katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi, hatua inayochangia kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za ujenzi.

“Mitambo tuliyonayo ni pamoja na mtambo wa kuchanganya zege (batching plant), malori ya kubeba mchanga, magari ya kubeba zege, mashine za kufyatua tofali pamoja na mitambo mingine mbalimbali. Mitambo hii inatusaidia kupunguza gharama za ujenzi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi,” amesema Mhandisi Chaula.

Aidha, amesema TBA inaendelea na mikakati ya kuongeza mitambo mipya ya kisasa ambayo, pamoja na kutumika katika utekelezaji wa miradi ya Serikali, itatumika pia kwa shughuli za kibiashara kupitia huduma ya ukodishaji wa mitambo.

Kwa mujibu wa Mhandisi Chaula, hatua hiyo itasaidia kuongeza mapato ya wakala na kuimarisha uwezo wake wa kutekeleza miradi kwa wakati na kwa ubora unaokidhi viwango vinavyohitajika.

Amesisitiza kuwa uwepo wa mitambo ya kutosha na ya kisasa ni nguzo muhimu katika kuhakikisha miradi ya ujenzi inakamilika kwa ufanisi, kwa wakati na kwa ubora

slot gacor