Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

MENEJIMENTI KUU YA TBA YAFANYA KIKAO KUELEKEA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Imewekwa: 03 December, 2025
MENEJIMENTI KUU YA TBA YAFANYA KIKAO KUELEKEA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Menejimenti Kuu ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imefanya kikao maalumu cha maandalizi kuelekea mkutano wa Baraza la Wafanyakazi unaotarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 2-3, 2025 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimeongozwa na Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro, ambapo wajumbe wamepitia kwa kina ajenda zitakazowasilishwa katika Baraza hilo ili kuhakikisha mkutano unafanyika kwa ufanisi na kufikia malengo yake.

Wajumbe walioshiriki katika kikao hicho ni sehemu ya wajumbe watakaoshiriki katika mkutano rasmi wa Baraza la Wafanyakazi, hatua inayoonesha dhamira ya TBA ya kuimarisha ushirikishwaji na uwazi katika masuala ya kiutendaji.