TBA YAZINDUA TOVUTI YAKE MPYA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro amezindua rasmi tovuti mpya ya TBA baada ya kukamilika kwa mchakato wa ujenzi wa tovuti hiyo ambayo imechukua nafasi ya tovuti ya zamani.
Tovuti hiyo imezinduliwa baada ya kupitia hatua muhimu za ujenzi zikiwemo ujenzi wa tovuti, uingizaji maudhui, ukaguzi wa maudhui zilizopandishwa, ukaguzi wa kiusalama, pamoja na kuipandisha kwa ajili ya matumizi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti hiyo Arch. Kondoro ameipongeza timu ya wataalam kutoka TBA na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) waliofanikisha ujenzi wa tovuti hiyo na kutoa wito kwa watumishi wote wa TBA kutoa taarifa sahihi na za uhakika ili ziwe zinapandishwa mara kwa mara na kuwawezesha watumiaji wa tovuti hiyo kupata taarifa sahihi na kwa wakati.
Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 18, 2025 katika Ukumbi wa ofisi ndogo za TBA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.