Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

TBA YASHIKA NAFASI YA PILI KATIKA TAASISI ZA UMMA KATIKA MAONESHO YA TISA YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI 2026 GEITA.

Imewekwa: 05 October, 2026
TBA YASHIKA NAFASI YA PILI KATIKA TAASISI ZA UMMA KATIKA MAONESHO YA TISA YA KITAIFA YA TEKNOLOJIA YA MADINI 2026 GEITA.

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeshika nafasi ya pili katika kundi la Taasisi za Umma katika Maonesho ya Tisa (09) ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini 2026 yanayofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hasan Bombambili Mkoani Geita.

Tuzo hiyo imetolewa na Mgeni Rasmi katika hafla ya ugawaji wa tuzo, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Muungano na Mazingira,  Dkt. Latifa M. Khamis ikiwa ni sehemu ya kutambua taasisi zilizofanya vizuri katika maonesho hayo kwa kuzingatia ubora wa huduma, uwasilishaji wa taarifa na namna ya kutangaza fursa na huduma wanazotoa.

Nafasi hiyo ya pili ni ishara ya jitihada na dhamira ya TBA katika kuendelea kuwa kinara wa utoaji wa huduma bora, pamoja na kuongeza uelewa wa umma kuhusu huduma, miradi na fursa mbalimbali za Uwekezaji zinazotolewa na TBA.

Kupitia ushiriki wake katika maonesho hayo, TBA imeendelea kutoa taarifa kuhusu huduma zake katika maeneo ya ujenzi, ushauri wa kitaalamu pamoja na uendelezaji na usimamizi wa miliki za Serikali. 

Aidha, TBA pia inaendelea kutumia majukwaa haya kuwaita wawekezaji kutoka Ndani na Nje ya Tanzania kuja kuwekeza kwa njia ya ubia (PPP) katika maeneo yake 38 ambayo yameiva  kwa ajili ya uwekezaji katika Mikoa 20 Tanzania Bara.

slot gacor