Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro, Amefungua rasmi Kikao Kazi cha Maandalizi ya Mpango na Bajeti (MTEF) 2026/27

Imewekwa: 17 February, 2026
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro, Amefungua rasmi Kikao Kazi cha Maandalizi ya Mpango na Bajeti (MTEF) 2026/27

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoro, leo Februari 16, 2026 amefungua rasmi Kikao Kazi cha Maandalizi ya Mpango na Bajeti (MTEF) 2026/27 kilichofanyika katika ukumbi wa Peacock Hotel Jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, ameeleza kuwa bajeti si takwimu pekee bali ni chombo cha kutekeleza dira na dhima ya TBA kwa vitendo. Amesisitiza umuhimu wa majadiliano ya kina kuhusu maoteo ya bajeti, vipaumbele vyenye kuleta matokeo chanya, ufanisi wa matumizi ya rasilimali pamoja na kuimarisha uwajibikaji na uwazi katika utekelezaji.

Aidha, amehimiza ubunifu na matumizi ya teknolojia kama nyenzo ya kuongeza mapato, kupunguza gharama na kuboresha huduma sambamba na kuzingatia miongozo na sera za kitaifa.

Kikao hiki ni hatua muhimu kuelekea utekelezaji wa Mpango Mkakati wa 2026/27-2030/31, kikilenga kuifanya TBA kuwa kinara wa uendelezaji na usimamizi wa Milki za Serikali kwa viwango vya juu vya weledi na ubora.