Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias
Kwandikwa ameipongeza TBA kwa kazi nzuri inayofanya katika Sekta ya Ujenzi kwa
kusimamia na kutekeleza Miradi ya Serikali kwa kuzingatia ubora na kwa gharama
nafuu. Na amewataka pia wadau wengine waje wajifunze TBA na kuwa wazalendo
katika kutekeleza miradi ya Serikali.
“Nakupongeza sana
Mtendaji Mkuu wa TBA, kwa kazi kubwa unayofanya katika kutekeleza Miradi ya
Serikali na kwa gharama nafuu, fedha mnayookoa inakwenda kusaidia huduma
zingine, hivyo Serikali iko pamoja navyi
na itaendelea kuwaunga mkono” Amesema Naibu Kwandikwa
Naibu Waziri Kwandikwa ametoa pongezi hizo kwenye Ziara ya
kutembelea Mradi wa Nyumba za makazi, Magomeni Kota unaotekelezwa na Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA).
Naye Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Elius Mwakalinga, amesema
kuwa katika kupunguza gharama, TBA imeamua kuwekeza katika vifaa na rasilimali
watu. Imefanikiwa kununua magari (Malori), mitambo na kuwa na wataalamu wa fani
mbalimbali za ujenzi wenye uwezo na weledi mkubwa katika utendaji kazi.
“TBA tunafanya kazi
kwa vitendo na hatuna tamaa na pesa, kikubwa ni Uzalendo tu” amesema
Mwakalinga
Mradi wa Magomeni ni mradi wa nyumba za Makazi