UTANGULIZI
Idara ya Miliki ni kati ya Idara kuu tatu zilizopo chini ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Idara hii inaongozwa na Mkurugenzi ambae anasaidiwa kusimamia na kutekeleza majukumu ya Idara kwa ushirikiano wa kitengo cha Usimamizi na Uendeshaji wa Miliki ya nyumba za Wakala, Kitengo kingine ni cha Utafiti na Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania. Aidha, ipo sehemu inayoshughulika na kuweka kumbukumbu za mikataba ya mauzo ya nyumba za Serikali.
Vitengo hivi vinaongozwa na wakuu wafuatao;
i. Msimamizi wa Nyumba - Chief Property Manager
ii. Msimamizi wa Utafiti na miradi ya Maendeleo Chief Research and Planning Development Manager.
iii. Msimamizi wa sehemu ya utunzaji wa kumbukumbu za miliki ya Serikali (Data Base Documentalist)
MAJUKUMU YA IDARA
Idara ya Miliki ina majukumu yafuatayo:
i. Kuhakikisha Wakala unamiliki maeneo kwa ajili ya ujenzi wa majengo na nyumba za watumishi wa umma.
ii. Ujenzi wa nyumba mpya za Serikali
iii. Uuzaji wa nyumba za Serikali kwa watumishi wa umma.
iv. Upangishaji wa nyumba za Serikali kwa viongozi na watumishi wa umma.
v. Uwekaji samani kwenye nyumba za Viongozi
vi. Upangishaji wa baadhi ya nyumba za Serikali kibiashara.
vii. Matengenezo ya nyumba/majengo ya Serikali.
viii. Kutoa ushauri kwa Serikali kuhusiana na masuala yanayohusu nyumba na usimamizi wa Miliki.
ix. Kutoa huduma ya usimamizi wa matumizi ya majengo ya Serikali yaliyokwisha kukamilika (Facility Management).
MAJUKUMU YA KITENGO CHA USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA NYUMBA
Kitengo cha usimamizi na uendeshaji wa milikikina majukumu ya kusimamia nyumba za viongozi, upangishaji wa nyumba kwa watumishi wa Serikali, kibiashara pamoja na uendeshaji wa nyumba hizo. Kitengo hiki pia kinasimamia matengenezo ya nyumba za Wakala.
MAJUKUMUYA KITENGO CHA UTAFITI NA MIRADI
Kitengo cha cha utafiti na miradi kina jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa viwanja pamoja na miliki zake kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Wakala. Kuandaa uchambuzi yakinifu wa ndani kwa miradi ya maendeleo ya wakala. Kusimamia nyumba/majengo yote yanayorejeshwa Serikalini chini ya wakala na majengo na viwanja vyote yanayomilikwa na Wakala na kusimamia uuzaji wa nyumba za Wakala.
Aidha, kitengo hiki kinatoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uthamini wa majengo na Ardhi ya Serikali
MAJUKUMU YA SEHEMU YA DATA BASE
Sehemu hii (Section) inasimamia uwekaji kumbukumbu
sahihi ya miliki ya Serikali ikiwa ni pamoja na nyumba zinazouzwa na kupangishwa
nchi nzima, viwanja na maeneo ya Serikali yaliyonunuliwa.