Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), imejipambanua katika kutoa huduma bora na yenye kukidhi viwango vinavyostahili. Jukumu kuu la Wakala wa Majengo Tanzania ni Usimamizi na Uendeshaji wa Miliki yote ya Serikali nchini. Jukumu hili limegawanyika katika maeneo mawili makubwa. Huduma ya Ushauri, Huduma ya ushauri wa michoro na makabrasha yanayotumika pamoja na usimamizi ikiwemo ushauri wa Kisera/Miongozo ya majengo ya Serikali na Uendeshaji wa Miliki.
Kuhusu
Usimamizi na Uendeshaji wa Miliki ya Serikali, TBA tumejikita katika kujenga na
kuwauzia nyumba za Serikali Watumishi wa Umma, kujenga na kuwapangisha
Watumishi wa Umma na wananchi wengine nyumba za Serikali, kutunza na kuweka
kumbukumbu za takwimu za majengo yote ya Serikali, kuzifanyia matengenezo
nyumba na majengo ya Serikali, kupata na kusimamia matumizi sahihi na endelevu
ya viwanja vya Serikali pia Kununua na kuweka samani zenye ubora kwenye nyumba
za Viongozi na majengo ya Serikali.
Hivyo
kufuatia adhima hii, TBA tumejiwekea mikakati zaidi, kuhakikisha kuwa tunafanikisha
miradi yote tunayotekeleza kwa kuzingatia ubora, gharama na muda wa kazi. Vyote
hivi vinaendana na dhamani halisi ya pesa (Value for Money) tunayowekeza katika
Miradi husika.
Kwa
muktadha huo TBA, tumejitahidi kuhakikisha kuwa tunakuwa na Menejimenti nzuri ya
Rasilimali watu ambayo imesheheni wataalamu wenye ujuzi na maarifa ya kutosha kulingana
na sifa ya Taasisi yetu. Kama TBA tunahakikisha kuwa watumishi tulionao
wanakuwa na maarifa na ujuzi sambamba na vitendea kazi vya kutosha, kwa hili TBA
tumepiga hatua kwa kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa watumishi wetu.
Pia TBA
tumefanikiwa kununua vifaa vya kisasa vinavyosaidia kuleta ufanisi katika kazi.
Vifaa hivi vinatuwezesha kujenga kwa
haraka, ubora na uhakika na matokeo yake ni unafuu kwa umaliziaji, usimamizi na
udhibiti wa ubora na gharama
Jambo
lingine, ni suala la uwajibikaji yaani “Commitment”. Katika hili TBA tumejitahidi
na bado tunaendelea kuhakikisha tunajenga moyo wa kujituma kwa wafanyakazi katika
utendaji kazi. Hili ni suala ambalo TBA tumeliwekea mkazo mkubwa na kulipa
kipau mbele. Tunaamini kuwa utaalamu na bidii ya kazi kwa kuzingatia maelekezo
yanayotolewa, hivyo hali hii inachangia kujenga maadili na nidhamu nzuri ya
kazi. Kazi bila nidhamu haiwezi kuwa bora na upungufu wa maadili unaharibu
utendaji kazi.
Tukizungumzia
zaidi kuhusu maadili, ni pamoja na kuwa na watumishi ambao wanafanya kazi kwa
uaminifu. Kwa kutambua hilo, TBA tunajitahidi kutekeleza majukumu yetu kwa kuhakikisha
kuwa tunazingatia mambo hayo makuu matatu ambayo ni utaalamu, bidii na maadili. Hii ndiyo nguzo yetu ya
kufanikisha mikakati yetu.