Akikabidhi nyumba hizo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa zaidi ya kaya 438 za watumishi wa umma watakaohamia Dodoma na wenye sifa ya kupatiwa nyumba na Serikali watakuwa na uhakika wa kupata nyumba hizo.
‘’Nyumba ambazo zinakabidhiwa kwa Wakala wa Majengo
ni nyumba za kuishi ambazo awali zilimilikiwa na Mamlaka ya Ustawishaji Makao
Makuu na kuhamishiwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma” Amesema Mhandisi Iyombe.
Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa TBA
Msanifu Majengo Elius Mwakalinga, ameshukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kuipatia TBA
nyumba hizo. Ameelezea kuwa nyumba hizo zitasaidia kupunguza tatizo la
nyumba kwa watumishi wa Serikali makao makuu Dodoma.
‘’TBA hapa Dodoma tulikuwa na nyumba takribani 400 katika maeneo ya Area D na Kisasa hivyo
kwa nyumba hizi sasa tutakuwa na nyumba takribani 800, lakini pia tuna programu
ya kujenga nyumba zingine 100 hadi 500 hapo baadaye” Amesema Mtendaji
Mwakalinga.
Aidha amebainisha kuwa
pamoja na kwamba nyumba zingine zinahitaji ukarabati, TBA itajitahidi
kuhakikisha kuwa zinakarabatiwa kuweza kumfanya mtumishi kukaa vizuri.
Jumla ya Nyumba 141 yakiwepo magorofa 45 yemekabidhiwa kwa wakala wa majengo Tanzania TBA kufuatia kuvunjwa kwa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao makuu CDA na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 15 Julai, 2017