• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • English

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaWakala wa Majengo Tanzania

  • kuhusu Sisi
    • Ujumbe kutoka kwa Mtendaji Mkuu
    • Sisi ni Nani
    • Dira na Dhamira
    • Tunafanya Nini
    • Mikakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Bodi ya Ushauri
    • Muundo wa Taasisi
    • Senior Management
    • Kurugenzi wa Uwezeshaji wa Huduma
    • Kurugenzi ya Ushauri
    • Kurugenzi ya Ujenzi
    • Kurugenzi ya Miliki
    • Meneja wa Mikoa
  • Nyumba
    • Nyumba za Kuuza
    • Nyumba za Kupangisha
    • Fomu ya Ununuzi wa Nyumba
    • Fomu ya ununuzi wa Nyumba
  • Miradi
    • Miradi Tunayoishikilia
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyo Katika usanifu
    • Miradi Tunayotegemea kufanya
  • Machapisho
    • Machapisho
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
  • Ununuzi
    • Mpango wa Manunuzi wa Mwaka
    • Mialiko ya zabuni
    • Orodha ya Wazabuni Walioshinda

Habari Mpya

  • SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWENYE UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI

    tokea mwezi 1
  • MENEJIMENTI YA TBA YAHIMIZWA KUKUTANA MARA KWA MARA.

    tokea mwezi 1
  • TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

    tokea mwezi 1
  • TBA NA ZBA KUENDELEZA MASHIRIKIANO

    tokea mwezi 1

Latest Press Release

WAZIRI BASHUNGWA ATEMBELEA TBA NA KUIPONGEZA.

Imewekwa: Friday 08, September 2023

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ametembelea Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya katika kutekeleza miradi ya Serikali hususani, ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma.

"TBA mnafanyakazi nzuri, tumeona katika ujenzi wa Ikulu ya Chamwino, Wajenzi walikuwa Suma JKT, na TBA mlikuwa Wataalamu na Washauri katika Mradi huo ambao umetekelezwa kwa ubora mkubwa". Anafafanua, Waziri Bashungwa.

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa rai kwa wapangaji wote waliopanga nyumba za TBA, kulipa madeni yao yote ya Kodi wanazodaiwa ili TBA iweze kutekeleza miradi mingine.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daudi Kondoro, ametaja kuwa TBA imekuwa ikidai kiasi cha fedha zaidi ya shilingi Bilioni 81 kwa washitiri mbalimbali na wapangaji wa nyumba hali inayokwamisha utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake.

Amebainisha kuwa TBA, imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya ushauri na ujenzi kwa ubora.

Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba 3500 za makazi kwa watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma, mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za Viongozi jijini Dodoma, nyumba za majaji katika mikoa minne. Miradi mingine inatekelezwa katika eneo la Temeke Kota, Magomeni Kota na Masaki jijini Dar es Salaam pamoja na Ghana Kota jijini Mwanza ambapo ujenzi wake unaendelea vizuri.

Ziara ya Waziri Bashungwa kutembelea TBA imelenga kujitambulisha, kujua shughuli zinazotekelezwa, mafanikio pamoja na dira ya mwelekeo katika utekelezaji wa kazi zake.

Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

TBA
THE CHIEF EXECUTIVE, TANZANIA BUILDINGS AGENCY (TBA), 13 MOROGORO ROAD, P.O BOX 94, 41102 VIWANDANI, DODOMA TANZANIA, EMAIL: ce@tba.go.tz Website: www.tba.go.tz
Nukushi :
Namba ya Simu : +255 733 483 437, +255 677 108 010
Barua Pepe : barua@tba.go.tz

Linki za Haraka

Linki Linganifu

  • WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Utumishi
  • Tume ya Takwimu ya Taifa
  • Tume ya Ajira

©2025 wakala wa majengo tanzania . Haki zote zimehifadhiwa..

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.Inaendeshwa na Wakala ya Majengo Tanzania