• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • English

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaWakala wa Majengo Tanzania

  • kuhusu Sisi
    • Ujumbe kutoka kwa Mtendaji Mkuu
    • Sisi ni Nani
    • Dira na Dhamira
    • Tunafanya Nini
    • Mikakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Bodi ya Ushauri
    • Muundo wa Taasisi
    • Senior Management
    • Kurugenzi wa Uwezeshaji wa Huduma
    • Kurugenzi ya Ushauri
    • Kurugenzi ya Ujenzi
    • Kurugenzi ya Miliki
    • Meneja wa Mikoa
  • Nyumba
    • Nyumba za Kuuza
    • Nyumba za Kupangisha
    • Fomu ya Ununuzi wa Nyumba
    • Fomu ya ununuzi wa Nyumba
  • Miradi
    • Miradi Tunayoishikilia
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyo Katika usanifu
    • Miradi Tunayotegemea kufanya
  • Machapisho
    • Machapisho
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
  • Ununuzi
    • Mpango wa Manunuzi wa Mwaka
    • Mialiko ya zabuni
    • Orodha ya Wazabuni Walioshinda

Habari Mpya

  • SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWENYE UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI

    tokea mwezi 1
  • MENEJIMENTI YA TBA YAHIMIZWA KUKUTANA MARA KWA MARA.

    tokea miezi 2
  • TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

    tokea miezi 2
  • TBA NA ZBA KUENDELEZA MASHIRIKIANO

    tokea miezi 2

Latest Press Release

KAMATI YA MIUNDOMBINU YASHAURI TBA UJENZI WA NYUMBA ZA KISASA

Imewekwa: Friday 02, September 2022

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha inajenga nyumba za kisasa ambazo zinaendana na uhalisia ili kukidhi mahitaji ya washitiri wake.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Suleiman Kakoso, mara baada ya Kamati hiyo kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Wakala huo.

Mheshimiwa Kakoso, amesema kuwa sambamba na hilo Wakala huo umetakiwa kuhakikisha unaongeza ubunifu katika utekelezaji wa miradi yake ili kuweza kukidhi soko la ushindani nchini na nje ya nchi.

“Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi yenu, ila hakikisheni mnaweka mikakati inayotekelezeka kwani uwekezaji kwenye ujenzi wa nyumba unakuwa na kubadilika kila siku hivyo mnatakiwa mwende sambamba na mabadiliko hayo ili kuweza kupata wateja ndani na nje ya nchi”, amesema Kakoso.

Aidha, Kakoso ameitaka TBA kuhakikisha wanaendeleza na kubuni miradi mbalimbali katika maeneo ambayo wanamiliki ili kulinda maeneo yao pamoja na kusambaza huduma maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesisitiza TBA kuendelea kuwa wabunifu kwa kuhakikisha unaendelea kujenga na kukarabati nyumba na majengo ya Serikali ili kuongeza ubora wa makazi kwa viongozi na watumishi wa umma.

Waziri Mbarawa ametaja miradi ya kitaifa mikubwa ambayo imetekelezwa na TBA kuwa ni ujenzi wa nyumba za makazi za Magomeni Kota, jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Sekou-Toure Mwanza, jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Ujenzi wa makazi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Usimamizi wa mradi wa ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imepokea, kujadili na kushauri taarifa ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

TBA
THE CHIEF EXECUTIVE, TANZANIA BUILDINGS AGENCY (TBA), 13 MOROGORO ROAD, P.O BOX 94, 41102 VIWANDANI, DODOMA TANZANIA, EMAIL: ce@tba.go.tz Website: www.tba.go.tz
Nukushi :
Namba ya Simu : +255 733 483 437, +255 677 108 010
Barua Pepe : barua@tba.go.tz

Linki za Haraka

Linki Linganifu

  • WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Utumishi
  • Tume ya Takwimu ya Taifa
  • Tume ya Ajira

©2025 wakala wa majengo tanzania . Haki zote zimehifadhiwa..

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.Inaendeshwa na Wakala ya Majengo Tanzania