Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga Januari 28, 2020 amezungumza na Menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhusiana na utendaji kazi wao, ambapo katika kikao hicho ameelezwa kuwa TBA inakabiliwa na changamoto kubwa ya mtiririko mzuri wa fedha kutoka kwa washitiri pamoja na kutolipwa kwa wakati madeni ambayo wanazidai Taasisi mbalimbali za Serikali. Vile vile alielezwa kuwa miradi ambayo imetekelezwa vizuri na kwa wakati ni ile ambayo inapata fedha kwa wakati. Katibu Mkuu aliiagiza Menejimenti ya TBA kuandaa taarifa na kuiwasilisha kwake juu ya sababu zinazofanya wasitekeleze miradi kwa wakati pamoja na mkakati waliomueleza wa namna ya kukabiliana na changamoto zilizoainishwa kwa ajili ya kuboresha utekelezaji wake.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro amemthibitishia Katibu Mkuu kuwa maelekezo yote ameyapokea na kuahidi kuyatekeleza.