Februari 2, 2023 Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umefanya kikao na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na Maafisa kutoka Benki ya Dunia chini ya uongozi wa Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud Kondoro.
Kikao hicho kililenga kuwapatia uzoefu maafisa wa TAMISEMI na Benki ya Dunia juu ya namna ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi zinazohusu jamii ya watu wengi wanaoishi pamoja kama ilivyokuwa kwa wakaazi 664 waliokuwa wakiishi katika eneo la Magomeni Kota.
Katika kikao hicho TBA ilipokea wasilisho la mpango wa uendelezaji wa eneo la Bonde la Mto Msimbazi na kutoa maoni yake kama mdau muhimu katika sekta ya majengo nchini.
Pia, TBA ilifanya wasilisho linaloelezea namna mradi wa ujenzi wa nyumba 644 za wakaazi wa Magomeni Kota ulivyotekelezwa.
TBA imetembelewa na maafisa hao kama Mdau mkubwa na muhimu katika Sekta ya Majengo nchini hasa kukiwa na maandalizi yakuanza uendelezaji wa bonde la mto Msimbazi.