Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea jengo la Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu na kuridhishwa na kazi iliyofanywa na TBA katika
kukamilisha mradi wa ujenzi wa majengo hayo. TBA ilikuwa mkandarasi katika Ujenzi
wa majengo ya Hospitali hiyo. Majengo yaliyojengwa na TBA yanajumuisha Jengo la
OPD, Jengo la Maabara ya Kisasa, Jengo la Mionzi na Upasuaji pamoja na Jengo la
kuunguzia taka. Mara baada ya kutembelea majengo mbalimbali katika Hospitali
hiyo, Makamu wa Rais alieleza kufurahishwa na kazi iliyofanywa na kuomba kupiga
picha na watumishi wa TBA.
Aidha Makamu wa Rais, Mhe.
Samia Suluhu Hassan baada ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
alieleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa kutokana na maendeleo ya kiutendaji
katika Hospitali hiyo.
Ziara hiyo ilifanyika Machi 07, 2020 kabla ya siku ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu Machi 08, 2020 ambayo mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.