Januari 03, 2022 Menejimenti ya TBA ikiongozwa na Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud W. Kondoro wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati wa nyumba na Majengo yaliyochini ya TBA katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. ukarabati huo ulihusisha kupaka rangi, ukarabati wa miundombinu ya maji safi na taka, Ukarabati wa mifumo ya umeme pamoja na ukarabati wa mapaa. Ambapo kwa sasa ukarabati huo kwa jijini Dar es Salaam umefikia hatua za mwisho.