Ujenzi wa nyumba 20 za viongozikatika eneo la Kisasa Jijini Dodoma umefikia asilimia 90 ambapo nyumba 14 zimekamilika na zingine 6 ziko katika hatua ya ukamilishaji. Ujenzi huo ulianza kutekelezwa Julai 2021 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Mhandisi Imabaraka Shedafa ambaye ni msimamizi wa mradi huu anasema kuwa kila nyumba ina vyumba 3 vya kulala, sehemu ya kujisomea, sebule, jiko pamoja na stoo
“Changamoto iliyokuwepo kuna kipindi mvua ilinyesha ikapelekea ujenzi kusimama kidogo, pia kulikuwepo na upungufu wa saruji katika maduka ya Dodoma hali iliyopelekea kuchelewa”. Anabainisha Bi. Victoria Tairo ambaye ni Mkadiriaji Majenzi (Qs) katika Mradi huo.
Aidha Ushirikiano wa kutosha upo baina ya mshitiri na TBA wanafanya kazi kwa ili kuhakikisha ujenzi unamalizika vizuri na kuwezesha viongozi kuingia katika nyumba hizo.