Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daud W. Kondoro amesisitiza juu ya zoezi muhimu kitaifa la Sensa ya Watu na Makazi ambalo litarajiwa kufanyika nchi nzima ifikapo Agosti 23, mwaka huu.
Akizungumza juu ya zoezi hilo Arch. Kondoro alisema "Tupo tayari kwenda kujiandikisha katika Sensa kwasababu ya umuhimu wa zoezi hilo hivyo kupitia kujiandikisha kwa upande wa huduma za Serikali ambazo zitatolewa kwa usahihi kwa kutambua idadi ya watu na mahitaji mengine kwa muujibu wa maswali yatakavyoulizwa kwenye Sensa"
Vile vile Arch. Kondoro amesisitiza kuwa kwa upande wa TBA ziimefanyika jitihada kubwa kufikisha habari kwa watumishi wa TBA nchi nzima kupitia Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Masoko kwa lengo la kuhakikisha watumishi wote wanashiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa.
Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linatarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022.