• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • English

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaWakala wa Majengo Tanzania

  • kuhusu Sisi
    • Ujumbe kutoka kwa Mtendaji Mkuu
    • Sisi ni Nani
    • Dira na Dhamira
    • Tunafanya Nini
    • Mikakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Bodi ya Ushauri
    • Muundo wa Taasisi
    • Senior Management
    • Kurugenzi wa Uwezeshaji wa Huduma
    • Kurugenzi ya Ushauri
    • Kurugenzi ya Ujenzi
    • Kurugenzi ya Miliki
    • Meneja wa Mikoa
  • Nyumba
    • Nyumba za Kuuza
    • Nyumba za Kupangisha
    • Fomu ya Ununuzi wa Nyumba
    • Fomu ya ununuzi wa Nyumba
  • Miradi
    • Miradi Tunayoishikilia
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyo Katika usanifu
    • Miradi Tunayotegemea kufanya
  • Machapisho
    • Machapisho
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
  • Ununuzi
    • Mpango wa Manunuzi wa Mwaka
    • Mialiko ya zabuni
    • Orodha ya Wazabuni Walioshinda

Habari Mpya

  • SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWENYE UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI

    tokea mwezi 1
  • MENEJIMENTI YA TBA YAHIMIZWA KUKUTANA MARA KWA MARA.

    tokea miezi 2
  • TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

    tokea miezi 2
  • TBA NA ZBA KUENDELEZA MASHIRIKIANO

    tokea miezi 2

Latest Press Release

NINAIPONGEZA TBA - RC SHIGELA.

Imewekwa: Monday 15, August 2022

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela amefanya ziara ya Kutembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato ambao unatekelezwa kwa awamu.

Akizungumza mara baada kukagua mradi huo Mhe. Shigela amesema anamshukuru Mhe. Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao unasaidia kutoa huduma ya afya kwa wakazi wa maeneo mbalimbali hususani wa Kanda ya Ziwa.

Vile vile Mhe. Shigela ameipongeza TBA kwa Ubunifu na ujenzi unaozingatia viwango vya ubora katika utekelezaji wa mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Martha Mkupasi amesema miradi mingi inayotekelezwa na TBA Wilayani Chato inajengwa kwa ubora unaotakiwa pamoja na kuzingatia muda wa mkataba.

Akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa mradi huo Meneja wa TBA Mkoa wa Geita Mhandisi Gladys Gefta amesema utatekelezaji wa mradi huo unafanywa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza imefikia asilimia 99 ukihusisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la Madawa na Maabara, jengo la wagonjwa wa dharura, jengo la wagonjwa mahututi, jengo la kuchomea taka pamoja na jengo la kangavuke ( Power house). Aidha Mhandisi Gefta amesema awamu ya pili imefikia asilimia 79 ikihusisha ujenzi wa jengo la wodi la ghorofa mbili, jengo la mionzi ( Radiology) pamoja na kazi za nje ( tenki la maji, vibanda vya walinzi, sehemu ya kuegeshea magari na marekebisho ya mandhari ya nje).

Vile vile Mhandisi Gefta amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo pamoja na kushukuru uongozi wa Mkoa wa Geita kwa ushirikiano wanaoutoa.

Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda - Chato unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania ( TBA) kama Mkandarasi na Mshauri Elekezi.

Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

TBA
THE CHIEF EXECUTIVE, TANZANIA BUILDINGS AGENCY (TBA), 13 MOROGORO ROAD, P.O BOX 94, 41102 VIWANDANI, DODOMA TANZANIA, EMAIL: ce@tba.go.tz Website: www.tba.go.tz
Nukushi :
Namba ya Simu : +255 733 483 437, +255 677 108 010
Barua Pepe : barua@tba.go.tz

Linki za Haraka

Linki Linganifu

  • WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Utumishi
  • Tume ya Takwimu ya Taifa
  • Tume ya Ajira

©2025 wakala wa majengo tanzania . Haki zote zimehifadhiwa..

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.Inaendeshwa na Wakala ya Majengo Tanzania