Waziri Mstaafu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ameguswa na TBA kwa kukamilisha na kukabidhi mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi za Magomeni Kota.
“Mimi kama Waziri mstaafu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, nawapongeza TBA kwa kukamilisha nyumba za makazi za Magomeni kota, mmetekeleza ahadi kwa zile Kaya 644, na kuwarejesha kuendelea kuishi”.
“Nawapongeza pia kwa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ihungo, nimefurahi kuona imekamilika na wanafunzi wanaendelea kusoma”.
“Nyumba ni kitu muhimu sana kwa wafanyakazi wa Serikali wakipata nyumba wanafanya kazi kwa bidii na tija ya kazi inaonekana”.
Profesa Tibaijuka ameeleza hayo baada ya kutembelea Banda la TBA kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.