• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • English

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaWakala wa Majengo Tanzania

  • kuhusu Sisi
    • Ujumbe kutoka kwa Mtendaji Mkuu
    • Sisi ni Nani
    • Dira na Dhamira
    • Tunafanya Nini
    • Mikakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Bodi ya Ushauri
    • Muundo wa Taasisi
    • Senior Management
    • Kurugenzi wa Uwezeshaji wa Huduma
    • Kurugenzi ya Ushauri
    • Kurugenzi ya Ujenzi
    • Kurugenzi ya Miliki
    • Meneja wa Mikoa
  • Nyumba
    • Nyumba za Kuuza
    • Nyumba za Kupangisha
    • Fomu ya Ununuzi wa Nyumba
    • Fomu ya ununuzi wa Nyumba
  • Miradi
    • Miradi Tunayoishikilia
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyo Katika usanifu
    • Miradi Tunayotegemea kufanya
  • Machapisho
    • Machapisho
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
  • Ununuzi
    • Mpango wa Manunuzi wa Mwaka
    • Mialiko ya zabuni
    • Orodha ya Wazabuni Walioshinda

Habari Mpya

  • SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWENYE UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI

    tokea mwezi 1
  • MENEJIMENTI YA TBA YAHIMIZWA KUKUTANA MARA KWA MARA.

    tokea mwezi 1
  • TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

    tokea mwezi 1
  • TBA NA ZBA KUENDELEZA MASHIRIKIANO

    tokea mwezi 1

Latest Press Release

TBA YAENDELEA KUJENGA MAJENGO DAR ES SALAAM

Imewekwa: Monday 16, October 2023

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umewahikishia wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kupata makazi bora yanayokidhi mahitaji ya teknolojia ya kisasa.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya nyumba za makazi katika Maeneo ya Temeke Kota, Magomeni Kota na Masaki Mkurugenzi wa Idara ya Miliki FRV. Said Mndeme amesema TBA imeazimia kutekeleza miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi ili kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba bora za makazi nchini.

Aidha, amesema anaishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kutenga fedha zaidi bilioni 60 ndani ya miaka miwili kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mpya za makazi.

"Katika eneo la Temeke Kota unaendelea ujenzi wa jengo moja la sakafu tisa (9) lenye uwezo wa kuchukua familia 144 ambapo mpango wetu kama Wakala ni kuhakikisha eneo hilo limakuwa na majengo saba yenye uwezo wa kuchukua familia 1008" amesema Mndeme.

Pia ametoa ufafanuzi juu ya miradi inayoendelea kutekelezwa katika maeneo ya Magomeni Kota awamu ya Pili na Msasani Peninsular Masaki kuwa katika maeneo hayo TBA inaendelea kuhakikisha inakamilisha majengo ya kisasa yatakayokuwa na huduma zote za msingi.

"Katika Maeneo ya Magomeni Kota na Canadian Masaki tumekamilisha majengo mawili ambayo yalizinduliwa na sasa tunaendelea na ujenzi wa ghorofa ambalo limefikia 83% na matarajio yetu mwezi Januari 2024 litaanza kutumika. Pia katika eneo la Masaki tunaendelea na ujenzi wa majengo mawili yenye uwezo wa kubeba familia 24 ambayo yamefikia 53%, ambayo tunatarajia kuwa na wakaazi 472 pamoja na uwepo wa maduka ya kisasa” amesema Mndeme.

Awali akizungumza Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam Arch. Benard Mayemba amesema miradi yote itakamilika kwa wakati kwa kuzingatia viwango vya ubora pamoja kuhakikisha mahitaji yote ya msingi yanazingatiwa ili nyumba hizo ziweze kwenda kutatua changamoto ya makazi kwa jamii iliyokusudiwa.

Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

TBA
THE CHIEF EXECUTIVE, TANZANIA BUILDINGS AGENCY (TBA), 13 MOROGORO ROAD, P.O BOX 94, 41102 VIWANDANI, DODOMA TANZANIA, EMAIL: ce@tba.go.tz Website: www.tba.go.tz
Nukushi :
Namba ya Simu : +255 733 483 437, +255 677 108 010
Barua Pepe : barua@tba.go.tz

Linki za Haraka

Linki Linganifu

  • WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Utumishi
  • Tume ya Takwimu ya Taifa
  • Tume ya Ajira

©2025 wakala wa majengo tanzania . Haki zote zimehifadhiwa..

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.Inaendeshwa na Wakala ya Majengo Tanzania