Zoezi la kuwaondoa katika nyumba za TBA wapangaji wanaodaiwa kodi za pango limeingia awamu ya pili ambapo kwa sasa linalenga Taasisi mbalimbali za Serikali mkoani Dodoma.
Qs. Emmanuel Wambura, Meneja wa TBA mkoa wa Dodoma amesema, kabla ya utekelezaji huu kuanza hatua mbalimbali zimefanyika ikiwemo kuwajulisha wahusika.
"Tuliwajulisha mapema kuhusu madeni wanayodaiwa na hatua ambazo tutachukua endapo hawatalipa, ndiyo maana tumeanza zoezi hili la kuwaondoa"
Wapangaji kutolipa kodi za pango kwa wakati kunachangia TBA kushindwa kutekeleza mipango yake ipasavyo.
Zoezi hili limeanza kwa nyumba zilizopo eneo la Kisasa na litaendelea kwa nyumba zote mkoani Dodoma