WAFANYAKAZI 10 wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wameshiriki mbio za riadha ya UDSM Marathon kwa lengo la kuweka vyema afya zao kama sehemu ya mazoezi kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza na pia kudumisha ushirikiano.
Hayo yamesemwa na Bw. Frank Kanyesi, ambaye ni Afisa Utumishi TBA Desemba 3, 2023 wakati waliposhiriki mbio hizo jijini Dar es Salaam.
Amesema mazoezi yanasaidia wafanyakazi kuwa imara zaidi kiafya, hivyo kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake kristolearachel Msengi mfanyakazi wa TBA amesema mbio hizo ni muhimu kwao na ndiyo sababu wameshiriki kwa wingi.
Mgeni rasmi katika mbio hizo alikuwa ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, ambapo kaulimbiu ilikuwa ni Kimbia Nasi Boresha Maisha ya Wanachuo.