Mafunzo hayo ya Mwezi mmoja yamewezeshwa katika vijiji vya Bwigili, Chahwa, Vikonje, Msanga, Kawawa na Chamwino. Lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia ujuzi wakazi hao ili kusaidia kutatua tatizo la ajira. Mafunzo yaliyotolewa ni pamoja na Ujenzi, Seremala, Mapishi, Ulinzi, Usafi na Mazingira.
Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Elius Mwakalinga
amewataka wanufaika wa mafunzo hayo kuzingatia maelekezo kutoka kwa wakufunzi
wao ili kila mmoja aweze kuelewa kile anachofundishwa kwa lengo la kuboresha
maisha yake.
Kwa upande wao wanufaika wa
mafunzo hayo, wameishukuru TBA kwa kuwezesha mafunzo hayo na kuahidi kuzingatia
maelekezo yote watakayopewa na wakufunzi wao.