Wakala wa Majengo Tanzanzia (TBA), kupitia Kikosi cha Ujenzi TBA Brigade, imezidi kujiimarisha kwa kuongeza Magari ambayo yatasaidia kuongeza na kuleta ufanisi katika utendaji kazi. Magari yaliyoletwa ni manne (Tipa) aina ya FAW kutoka Kampuni ya GF& Equipment LTD. Hii yote ni jitihada kubwa inayofanywa na TBA kuhahakisha kuwa inakuwa Mitambo yake ya kutosha na yenye uhakika.