Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inatimiza mwaka mmoja tangu ilipoingia madarakani March 19, 2021 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia kifo cha mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. katika kipindi hiki cha mwaka mmoja tumeshuhudia mambo makubwa ikiwemo uendelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanza toka Serikali ya Awamu ya tano. Kupitia TBA, Serikali ya sita imefanikiwa kutekeelza miradi mbalimbali ya majengo kwa ajili ya sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, ofisi, makazi ya viongozi na watumishi wa umma kwa gharama nafuu na katika ubora unaotakiwa.