Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
imeshiriki katika Maonyesho ya 25 ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi Kitaifa
(Nanenane) yalifanyika katika viwanja vya Nyakabindi-Bariadi mkoani Simiyu kuanzia
Agosti 3 hadi Agosti 11, 2018.
Lengo kuu la kushiriki Maonyesho hayo
ilikuwa ni kujitangaza, kutoa elimu juu ya huduma inazotoa pamoja na kukutana
na wadau mbalimbali wakiwemo washitiri ili kuongeza na kufungua fursa mpya za
kibiashara na huduma inazozitoa
Katika Maonesho haya TBA ilifanikiwa kushinda zawadi ya mshindi wa kwanza kwenye kipengele cha “Wakala wa Serikali”. Kauli mbiu ya Maonyesho ilikuwa “Wekeza katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda”.