Shirikia la Utangazi Tanzania (TBC) limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazalishaji wa vipindi vya elimu kwa Umma ambapo Wizara, Taasisi, Wakala na Mashrika mbalimbali ya Serikali hushiriki kwa lengo la kujengewa uwezo katika masuala ya uzalishaji wa vipindi vya elimu kwa Umma.
Februari 24, 2023 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano wa 107 wa mafunzo kwa wazalishaji wa vipindi vya elimu kwa umma.
Katika kuhitimisha mafunzo hayo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umepokea tuzo na cheti kwa kutambua mchango wake katika kufanikisha mafunzo hayo ambapo TBA ilikuwa mdhamini mkuu.
Mafunzo hayo yalidumu kwa kwa siku tano ambapo yalianza Februari 20 – 24, 2023 Mjini Morogoro.