Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unaandaa Mpango
Mkakati mpya hii ni baada ya Mpango Mkakati wa awali kuisha muda wake. Sehemu ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini chini ya Idara ya Huduma za Biashara kimeunda
timu ya kuandaa Mpango Mkakati ikihusisha wawakilishi mbalimbali wakiwemo Mwakilishi kutoka Wizarani (DTES), Wakurugenzi wa Idara, Mameneja wa Vitengo/ Sehemu, baadhi ya Mameneja wa Mikoa, Maafisa wa TBA pamoja na Muwezeshaji
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi
hicho Mkurugenzi wa Huduma Wezeshi Bw. Amos Nnko alisema, Mpango Mkakati huo ni
lazima uendane na Sera za Nchi na kuhakikisha unakidhi mahitaji ya Watumishi wa
Umma na Unaleta tija kwa TBA.
Mpango mkakati huo unatarajiwa kuleta mabadiliko chanya Katika utekelezaji wa kazi za TBA ili iweze kutimiza malengo yake kwa Ufanisi na kwa gharama nafuu.