• Maswali
  • Wasiliana Nasi
  • English

Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaWakala wa Majengo Tanzania

  • kuhusu Sisi
    • Ujumbe kutoka kwa Mtendaji Mkuu
    • Sisi ni Nani
    • Dira na Dhamira
    • Tunafanya Nini
    • Mikakati
    • Mkataba wa Huduma
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Bodi ya Ushauri
    • Muundo wa Taasisi
    • Senior Management
    • Kurugenzi wa Uwezeshaji wa Huduma
    • Kurugenzi ya Ushauri
    • Kurugenzi ya Ujenzi
    • Kurugenzi ya Miliki
    • Meneja wa Mikoa
  • Nyumba
    • Nyumba za Kuuza
    • Nyumba za Kupangisha
    • Fomu ya Ununuzi wa Nyumba
    • Fomu ya ununuzi wa Nyumba
  • Miradi
    • Miradi Tunayoishikilia
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Iliyo Katika usanifu
    • Miradi Tunayotegemea kufanya
  • Machapisho
    • Machapisho
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
  • Ununuzi
    • Mpango wa Manunuzi wa Mwaka
    • Mialiko ya zabuni
    • Orodha ya Wazabuni Walioshinda

Habari Mpya

  • SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWENYE UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI

    tokea mwezi 1
  • MENEJIMENTI YA TBA YAHIMIZWA KUKUTANA MARA KWA MARA.

    tokea miezi 2
  • TBA YAKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA JAPAN.

    tokea miezi 2
  • TBA NA ZBA KUENDELEZA MASHIRIKIANO

    tokea miezi 2

Latest Press Release

TBA fikirieni Mikakati mipya yenye ubunifu- Dkt. Mahenge

Imewekwa: Thursday 30, January 2020

Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wametakiwa kubuni Mikakati mipya yenye ubunifu (innovation) ambayo itawawezesha kutekeleza kwa ufanisi malengo yao. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binirith Satano Mahenge katika Hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TBA unaofanyika Dodoma.

“TBA mmepewa dhamana kubwa ya kutekeleza miradi mikubwa na nyeti yenye sura ya kitaifa na ambayo ina mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa letu, hivyo mnatakiwa kufanya kazi kwa kujituma badala ya mazoea ili kufikia malengo”

Aidha Dkt. Mahenge amewataka wafanyakazi hao kutumia Baraza hilo kutazama kwa undani hatua ambazo TBA imepiga na kujadili maeneo ambayo malengo ya TBA hayajafikiwa kwa lengo la kuboresha zaidi na kufikia malengo yaliyokusudiwa na Wakala.

Awali akizungumza katika Mkutano huo Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro amesema TBA imeendelea kutekeleza miradi ya Washitiri ambayo imegawanyika katika makundi manne (4); Miradi ya Ushauri, Miradi ya Ujenzi, Miradi ya usanifu na ujenzi na Miradi ya Usimamizi. Hadi kufikia Desemba, 2019, TBA imetekeleza jumla ya miradi 169.

Baadhi ya Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Radar katika viwanja vya ndege vya DSM, Songwe, KIA na Mwanza, Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Ujenzi wa jengo la Maabara, jengo la upasuaji na mionzi na jengo la wagonjwa wa nje kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu. Miradi mingine ni Ujenzi wa Vihenge vya kuhifadhia nafaka katika Mikoa ya Ruvuma, Njombe, Rukwa, Katavi, Manyara, Dodoma na Shinyanga pamoja na Mradi wa Ujenzi wa kituo cha pamoja cha Forodha Kasumulu-Mbeya.

Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Wakala wa Majengo Tanzania hufanyika mara 2 kwa Mwaka kwa lengo la kujadili maendeleo ya Wakala.

Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

TBA
THE CHIEF EXECUTIVE, TANZANIA BUILDINGS AGENCY (TBA), 13 MOROGORO ROAD, P.O BOX 94, 41102 VIWANDANI, DODOMA TANZANIA, EMAIL: ce@tba.go.tz Website: www.tba.go.tz
Nukushi :
Namba ya Simu : +255 733 483 437, +255 677 108 010
Barua Pepe : barua@tba.go.tz

Linki za Haraka

Linki Linganifu

  • WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Utumishi
  • Tume ya Takwimu ya Taifa
  • Tume ya Ajira

©2025 wakala wa majengo tanzania . Haki zote zimehifadhiwa..

Imesanifiwa, Imetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.Inaendeshwa na Wakala ya Majengo Tanzania