Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imefanikiwa kupata Kikombe cha ushindi kwenye Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoandaliwa na TANTRADE. Katika Maonyesho hayo yaliyofanyika kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2018 katika viwanja vya maonesho vya Mwl. J.K. Nyerere (sabasaba), TBA ilifanikiwa kushinda zawadi ya mshindi wa kwanza yaani “Certificate of Award as First Winner Prize under the category of Construction and Related Building Materials Exhibitors”. Pia TBA ilifanikiwa kupata cheti cha ushiriki wa Maonyesho hayo.
Lengo kuu la TBA kushiriki maonesho hayo ilikuwa ni kujitangaza, kutoa elimu juu ya
huduma zinazotolewa na wakala pamoja na kukutana na wadau mbalimbali ili kuongeza
fursa za kibiashara na huduma zinazotolewa na Wakala wa Majengo (TBA).
Katika Maonyesho
hayo, TBA ilionyesha baadhi ya Mitambo yake inayotumika katika Miradi
mbalimbali inayotekeleza nchi nzima. Pia baadhi ya michoro ya Majengo
inayojenga na mingine iliyokamilika.
Wananchi wengi waliotembelea
Banda hilo walifurahi kujifunza na kuona huduma zinazotolewa na TBA, hivyo
baadhi yao walipendekeza huduma ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma
uendelee kutekelezwa katika mikoa yote ya Tanzania.