Mnamo Juni 17, 2022 Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ulikabidhiwa rasmi nyumba kumi na moja (11) zilizokuwa zikitumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) baada ya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mpanda - Kibo - Usimbili.
Makabidhiano hayo yalihudhuriwa na Mgeni rasmi Bw. Chotto Sondo (Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali) ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango. Kwa upende wa TBA, Mtendaji Mkuu aliwakilishwa na Meneja wa TBA Mkoa wa Katavi Arch. Henrico Bahati.