TBA YAKAMILISHA MRADI WA UJENZI WA OFISI ZA TFS MKURANGA - PWANI
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)
umekamilisha na kukabidhi Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Wakala wa Misitu Tanzania
(TFS) Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. TBA imeshiriki ujenzi huo kama Mkandarasi
na Mshauri Elekezi. Ujenzi huo ulihusisha ujenzi wa jengo lenye ofisi kumi na
moja (11), maktaba, ukumbi wa mikutano pamoja na jiko. Katika ujenzi huo TBA imejenga
jengo la kisasa lenye ubora wa hali ya juu pamoja na kuzingatia uwepo wa miundombinu
ya watu wenye mahitaji maalumu.
Ukamilishaji wa mradi huo
utatatua changamoto ya uhaba wa ofisi kwa wafanyakazi wa TFS wilayani Mkuranga
na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao. Pia wananchi watapata huduma kwa
urahisi zaidi kutokana na uwepo wa ofisi zenye nafasi na miundombinu yote
muhimu.
TBA ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2002 kwa lengo la kusimamia miliki za Serikali.