TBA YATEKELEZA MIRADI MKOANI MBEYA
Wakala
wa Majengo Tanzania (TBA) umetekeleza miradi mbalimbali Mkoani Mbeya. Miradi
iliyotekelezwa inajumuisha miradi ya Ujenzi, Ushauri na ukarabati.
Meneja
wa TBA Mkoa wa Mbeya Mhandisi Jafari S. Kiyoga, ameitaja miradi ya ujenzi inayotekelezwa
mkoani humo kuwa ni Ujenzi wa jengo la Maktaba ya Chuo cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya (MUST), Ujenzi wa jengo la Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya
kanda Mbeya, Ujenzi wa jengo la upasuaji na jengo la Wodi ya wagonjwa wa Upasuaji
katika ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Pia
aliitaja miradi ya ushauri kuwa ni Ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Uyole,
Ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Chunya, Ujenzi wa ofisi za bonde la
ziwa Rukwa, Ujenzi wa jengo la Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mbeya, na
ujenzi wa mgahawa na fensi katika ofisi za TFS za kanda. Vile vile aliutaja Mradi
wa ukarabati kuwa ni Maboresho ya jengo la intern kuwa Ward Grade 1 katika Hospitali
ya rufaa ya Kanda Mbeya. Vile vile aliutaja mradi unaotarajiwa kuanza hivi
karibuni kuwa ni mradi wa ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Akiongea juu ya ukarabati wa karakana katika
mkoa wake, Meneja wa TBA Mkoa wa Mbeya amesema kuwa pindi ukarabati utakapokamilika
watakuwa na uwezo wa kuzalisha samani nyingi za kisasa zitakazotumika kwenye
miradi mbalimbali inayotekelezwa katika mikoa ya jirani, kuongeza mapato ya TBA
na kutoa nafasi za ajira kwa watanzania.
Akizungumzia juu ya ujenzi wa jengo la Maktaba
ya MUST, Makamu Mkuu wa Chuo Prof.
Aloyce Mvuma alisema anapongeza jitihada zilizofanywa na TBA katika
ujenzi wa jengo hilo ambalo limekamilika kwa asilimia 97 na lina uwezo wa kupokea
wanafunzi wengi kwa wakati mmoja kinyume na jengo lililokuwepo hapo awali. Pia Prof.
Mvuma alisema Maktaba hiyo imesanifiwa katika muundo wa kipekee kabisa tofauti na
maktaba nyingine kwani inauwezo wa kuratibu shughuli nyingi kwa wakati mmoja bila
kuwa na muingiliano wowote. Aidha, Prof. Mvuma amepongeza ushirikiano uliooneshwa
na ofisi ya TBA Mkoa wa Mbeya kwa kipindi chote cha ujenzi.